NADHARIA KATIKA SEMANTIKI
Kutokana na ugumu wa kufasili maana ya maana katika taaluma ya
semantiki ambayo ni tawi la isimu ambalo hujihusisha na uchunguzi wa lugha
katika maana hususani maana ya msingi, taaluma hii hushughulikia maana za
maneno na sentensi katika lugha mahususi na maana hizo hushughulikiwa
kisayansi.
Maana katika semantiki ilianzakushughulikiwa tangu enzi za Plato,
Aristotle, wataalamu mbalimbali walishughulikia falsafa, mantiki, saikolojia,
isimu na Athropolojia. Kila taaluma ilitofautiana, kulikuwa na tofauti ya isimu
na taaluma nyingine. Tofauti ya isimu na taaluma nyingine ni kwamba isimu
iliangalia maana kisayansi na usayansi huo ulikuwa wa kiupangilifu, kiuakinifu
kwa kutumia kanuni mbalimbali, ingawa walitumia kanuni bado kulikuwa na
matatizo mbalimbali.
Swali
Kwa nini bado kulikuwa na matatizo ya kufasili maana ya maana?
Jibu: maana ilichukuliwa kama kitu
ambacho akijatengamaa na kilikuwa tepetepe ama telezi kwani huwezi kukishika,
kinateleza. Mfano maji huchukuliwa katika kikombe na maana hasa hutegemea sana
uwezo na ufafanuzi wa msemaji kwa mantiki hiyo maana hufananishwa na kinyonga,
maana hutegemea muktadha wa mzungumzaji. Wanahisimu wanaona kuwa maana ni kitu
muhimu katika mawasiliano na maana inapokuwa tege mawasiliano huwa si kamili na
hakika mawasiliano bila maana si kitu. Kwa maana hiyo maana ni muhimu sana
katika mawasiliano kwani kuna kuwa na kitu ambacho mzungumzaji amekusudia
kukisema.
Maana ya maana
Habwe na Karanja (2007), wanasema neno maana lina fahiwa nyingi watu
wa kawaida wamelitumia kumaanisha vitu mbalimbali.
Mfano i/ una maana gani kufika umechelewa?,
ii/ yale mawingu meusi yana maana mvua itanyesha sasa,
iii/ mtu huyu hana maana yoyote,
iv/ manyunyu ina maana, mvua inayonyesha kidogokidogo,
v/ kuna joto,
vi/ kicheko katika mashetani kina maana gani?,
vii/ Aota maana yake ni mshipa mkubwa utokao moyoni na kupeleka damu
sehemu za mwili,
viii/ msaada wako una maana sana kwetu. Sentensi hizi zina maana
mbalimbali kama vile sababu, dalili, ishara, hafai, ufafanuzi, hali, kejeli,
umuhimu. Swali katika tungo hizo ni maana ipi inayohusu maana ya msingi katika
muktadha wa semantiki. Matumizi mapana na hivyo ni tata ili kuweka mipaka ya
semantiki ni muhimu kubainisha maana ya maana ya semantiki.
Kutokana na utata wa maana kuliibua nadharia mbalimbali ambazo kwa
kiasi fulani zimejikita katika kupunguza utata huo wa kuelezea maana ya maana.
Katika mjadala huu nadharia bainishi kama vile urejeleo, nadharia tumizi,
taswira/dhana, vichocheo mwitikio, vijenzi semantiki.
UREJELEO
Nadharia hii iliasisiwa na Ogden, C.K na Richards, I. A. Nadharia
hii inahusu uhusiano baina ya kiambo cha lugha na kitu au vitu katika ulimwengu
wa masilugha. Kwa mtazamo huu maana ya neno ni kitu halisi kinachorejerewa na
neno. Maneno ni majina ambayo dhima yake ni kutaja vitu. Maana ya neno ni
uhusiano baina ya neno hilo na kitu au vitu ambavyo neno hilo hurejelewa. Kwa
mfano, kitabu, simu n.k.
UPUNGUFU
i/ si kilia kiambo au leksimu yenye maana ina kirejerewa chake.
Mfano, katika lugha
kuna vinyambo ambavyo havina kirejeleo. Kama
vile Mungu, upepo, shetani, (dhana).
ii/ haifanyi kazi kwa maneno yenye uhusiano wa kipolisemia. Kwa
mfano Kichwa ni
leksimu yenye kuchanuza
maana nyingi.
iii/ Haifanyi kazi kwa maneno yenye uhusiano wa kihomonomia. Kama
vile kaa, chunga,
chungu, n.k.
iv/ pia haiwezi kufanya kazi katika maneno yenye uhusiano wa
kisinonimia, vinyambo
zaidi ya kimoja (kisawe).
NADHARIA YA DHANA / TASWIRA
Nadharia hii inafafanua kuwa maneno ya kiambo ni dhana au taswira
inayoibiliwa na kiambo hicho akilini mwa mwanalugha pindi kiambo hicho
kinapotumika.
Neno – kisemo- sentensi, kisemo ni dhana ijengekayo akilini mara tu
msemaji au msikilizaji anapozungumza ama kusikiliza, pia nadharia hii uhusisha
maana na wazo, uhusisha maana na kitu moja kwa moja hivyo inasaidia kutoa
majibu ya vinyambo visivyoweza kurejelewa.
MAPUNGUFU
·
Si bainifu na haiwezi
kuchunguzika, kutabili chochote, mwanaisimu hawezi kufanya utafiti wa aina
moja.
·
Picha za akilini ni dhahania ya
kutosha kuweza kuwakilisha maana za nomino au vitenzi vya kawaida.
·
Hakuna picha za jumla ya mguso.
·
Si kila kiambo kinahusiana na
taswira.
·
Haiwezi kuelezea viambo viwili
kuwa ni kisawe. Kinyambo huwa na taswira moja haina visawe.
·
Haiwezi kuelezea maana ya
sentensi au nahau.
NADHARIA TUMIZI
Nadharia hii iliasisiwa na mwanafalsafa mashuhuri
aliyejulikana kwa jina la Ludwing Wittgenstein mwaka 1930, alitamka kwa mifano
mingi ya maneno kuwa maana ya
neno ni matumizi yake katika lugha, msisitizo wake upo
katika maana ya neno au kisemo kilichotumika katika muktadha maalumu. Mtaalamu
huyu anaona kuwa maana ya neno ni matokeo au athari inayotokana na matumizi.
Hata hivyo si muhimu kuuliza maana ya neno bali matumizi yake katika muktadha
husika.
Nadharia hii imepunguza matatizo katika nadharia
tangulizi kwani watoto wanapojifunza lugha hujifunza maana ya viambo vya lugha
kutokana na jinsi vinyambo hivyo vinavyotumika na wanalugha wa jamii.
NADHARIA NA MATATIZO
Ø Si kweli kuwa maana ya matumizi ya neno hupatikana katika matumizi
ya neno,
Ø Inahalalisha tabia ya mabadiliko ya maana kutokana na muktadha.
Ø Huifanya maana iwe mali ya kundi fulani.
NADHARIA YA VICHOCHEO MWITIKO
Nadharia hii iliasisiwa na mtaalamu ajulikanaye kwa jina la
Bloomfield 1933, nadharia hii imejikita hasa katika kuchunguza maana ya umbo la
kiisimu na hali ambamo msemaji hutamka umbo hilo na mwitiko huibuliwa na
msikilizaji. Maana ni kichocheo cha msemaji na mwitiko wa msikilizaji. Mtaalamu
huyu anadai kuwa maana ya kisemo huwa katika muundo wa tendo uneni.
CHOCHEO →MWITIKO………CHOCHEO → MWITIKO
Kasekwa anaumwa njaa, anaona tofaa mtini(hali ya msemaji) anatamka
kuwa anataka tofaa (mwitiko wa msemaji)
NJAA
ANATAKA
↓
↓
CHOCHEO MWITIKO
Kapele anachochewa kuitika kwa kuruka ua, anaruka ua anapanda mti
anachuma embe na kuliweka mikononi mwa kasekwa.
CHOCHEO → MWITIKO
NJAA → NATAKA
CHAKULA → KUPOKEA
Matatizo ya nadharia
v Unaweza kueleza maana chache za kisemo cha lugha kwa kuwa hali
nyingi za matumizi zimechanganyikana, semo nyingi za lugha hazithibitiwi na
kichocheo katika muktadha zitokanamo. Kwa mfano mtu akiulizwa swali si lazima
atoe jibu.
v Maneno mengi hayataji vitu vionekanavyo au nduni zionekanazo , mfano
njaa.
v Wanalugha hawapokei maneno kwa vitu vinavyowakilisha maneno hayo.
v Maneno dhahania hayaelezeki katika nadharia hii. Mfano njaa.
VIJENZI SEMANTIKI
Hudai kuwa leksimu zote zaweza kuchanganuliwa kwa
kuzingatia seti si ukomo ya vijenzi semantiki ambavyo ni jumla. (Crystal, 1969)
uchanganuzi wa vijenzi semantiki ni mkabala uanochunguza leksimu tu. Mfano
mwanamke, fahiwa ya leksimu hii ina vijenzi vitatu ambavyo kwa hakika ni;
i.
Mtu
ii.
Mtu mzima
iii.
me
Ufafanuzi
i.
MWANAMKE = [+MTU], [+MTU
MZIMA], [-ME]
ii.
MSICHANA = [+MTU], [-MTU
MZIMA], [-ME]
iii.
MWANAMUME = [+MTU], [+MTU
MZIMA], [+ME]
Kadhalika vijenzi semantiki huwa na jozi kinzani, jozi hizo
huoneshwa kwa alama ya toa na jumlisha. Kijenzi mtu ni cha jimla kinahusisha
leksimu hiyo na leksimu kinzani. Leksimu kinzani, mti, majani, vijenzi
semantiki vya kijumla kama [MTU], [KITU], [OEVU] n.k. hutumika kupambanua
leksimu zilizo katika makundi tofautitofauti ya maana. Dhima kuu ya vijenzi
semantiki ni kupambanua leksimu zilizo katika kikoa kimoja cha maana. Kijenzi
semantiki [ME] na [MTU MZIMA] tunaweza kufafanua maana za mwanamke, mwanamume,
mvulana pamoja na msichana maneno haya ni vikoa vya maneno sawa.
Kwa mfano;
MWANAMKE
a.
MWANAMKE [- ME], [+MTU MZIMA]
b.
MWANAUME [+ME], [+MTU MZIMA]
c.
MVULANA [+ME], [-MTU MZIMA]
d.
MSICHANA [-ME], [-MTU MZIMA]
Upambanuzi huu unaonesha
kuwa leksimu mwanamke inatofautiana na leksimu mwanamume kwa kutoa [-ME],
leksimu msichana inatofautiana na leksimu mvulana kwa kutoa alama [-ME], pia
leksimu mvulana inatofautiana na leksimu msichana kwa kujumlisha [+ME]
Mfano undugu wa damu.
Baba
Mama
Shangazi
Mjomba
Kaka
Dada
Mwana
Binti
Mpwa
Binamu
Maneno haya ya
udugu wa damu ni tofauti na maneno mengine kwa kuwa yenyewe yanarejelewa
kiwakilishi cha msemaji. Maneno hayo yanaweza kuwakilishwa kwa kijenzi kimoja
ndugu na ili kukitofautisha ni lazima kiwe na kijenzi kingine.
Kwa mfano
[+me], [+mzazi], [mlalo], [mfuatano]
Baba [+me], [+mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Mama [-me], [+mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Shangazi [-me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Mjomba [+me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Kaka [+me], [-mzazi], [+mlalo], [+mfuatano]
Dada [-me], [-mzazi], [+mlalo], [+mfuatano]
Binti [-me], [-mzazi], [-mlamlo], [-mfuatano]
Mwana [+me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Mpwa [-/+me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Binamu [-/+me], [mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
ULALO ngazi ya
uhusiano wa usawa.
MFUATANO
uhusiano wa wima.
Swali muhimu
Jadili ugumu
unaojitokeza katika kufasili maana ya maana kwa kuzingatia nadharia za maana.
MAPUNGUFU YA KIJENZI SEMANTIKI
i.
Kutokuwepo kwa vijenzi vya
uteuzi wa vijenzi, kwa hawajaeleza wazi ni kwanini wanatumia me na ke, kijenzi
mlalo, na wima na si vinginevyo. Mzazi na mafuatano. Hivyo ni muhimu kueleza
kwanini vigezo hivyo vimetumika.
ii.
Mkabala huu unatumia mbinu ya
uwili ukinzani ambao unawakilishwa na alama za kujumlisha na kutoa. Unaweza
kufaa kwa leksimu ambazo vijenzi vyake vinaweza kubainika kwa urahisi. Lakini
pia unweza kufaa Zaidi katika leksimu nyingine kama vile viwakilishi.
iii.
Hakuna kikoa cha vijenzi
semantiki hivyo hakuna kigezo maalumu kinachoweza kueleza idadi ya vijenzi
semantiki.